Trending News

CCM Adverts and Promo

Monday, May 9, 2016

VIFAA VYA KUJIFUNGULIA WAJAWAZITO KUTOLEWA BURE

Serikali imetangaza kutoa bure vifaa vya kujifungulia wajawazito katika hospitali zote za umma nchini. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu meyasema hayo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kumpongeza Makamu wa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika nafasi hiyo.

Mkutano huo umeandaliwa na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT). Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na itatoa vifaa bure kwa wanawake wanaokwenda kujifungua na kwamba serikali imejipanga kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

No comments:

Post a Comment