![]() |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba
akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
![]() |
|
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt.
Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
![]() |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara
baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.
Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu wa kuuza madawa ya kulevya
kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za
kujiingizia kipato.
Waziri Nchemba ametoa agizo hilo
mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga
ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa
atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya
inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.
Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wataalum
wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo
hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.
Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa
Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili vyama vya
ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika miaka ya hivi karibuni.
Mawaziri walioapishwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar
es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo
na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh.
Charles Kitwanga.







No comments:
Post a Comment