![]() |
| Mkuu wa Kambi ya Nduta, Peter Buluku akiendelea na kazi zake za kila siku kwenye Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya ndani iliyopo ndani ya Kambi hiyo,wilayani Kibondo, Mkoa wa Kigoma. |
Na
Jacquiline Mrisho - Kibondo.
Kambi
ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma imewatengea eneo
maalumu la kuishi watu wenye ulemavu wa ngozi ili kulinda usalama wa maisha
yao.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kambi hiyo, Peter Buluku alipokuwa akiongea na mwandishi wa
habari hii juu ya maisha halisi ya wakimbizi hao wanaoishi katika kambi hiyo
wakitokea nchini Burundi.
Buluku
amesema kuwa katika kambi hiyo kuna baadhi ya wakimbizi wanaojihusisha na
vitendo vinavyohatarisha usalama wa wakimbizi wenzao vikiwemo vya ubakaji, wizi
na kujaribu kuteka watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mkuu
huyo wa kambi amefafanua kuwa mnamo mwezi Aprili mwaka huu, familia moja yenye
mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ilivamiwa na watu wasiojulikana na kumchukua
mtoto huyo lakini kwa bahati nzuri majirani walijitahidi kupiga kelele hivyo,
watuhumiwa waliamua kumtelekeza mtoto huyo na kukimbilia kusikojulikana.
"Kutokana
na kujitokeza kwa hali hiyo, Sisi pamoja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali
yanayotoa huduma kambini hapa tuliamua kuwatengea eneo maalumu lililo
karibu na kituo cha polisi watu hawa wenye ulemavu wa ngozi ili wawe na ulinzi
wa kutosha hivyo kuishi kwa amani kama binadamu wengine", alisema Buluku.
Hadi
sasa kambi hiyo ina jumla ya watu watano wenye ulemavu wa ngozi kutoka kwenye
familia mbili tofauti, Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani (UNHCR) limehaidi
kujenga jengo la kudumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu huo.
Kambi
ya Nduta ilianzishwa rasmi mwaka 1998 na kufungwa mwaka 2009. Ilifunguliwa kwa
mara ya pili mwaka 2015 baada ya kutokea kwa vurugu nchini Burundi na
kusababisha baadhi ya raia wa nchi hiyo kukimbilia nchini Tanzania, hadi sasa
kambi hiyo ina jumla ya wakimbizi 55,320 ambao ni raia wa Burundi.

No comments:
Post a Comment