Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali, Said Mohamed (kushoto) na
Balitiamo Damian waliolazwa katika
taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake
aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali, Isaya Sanga (katikati) na
Abasi Bushole waliolazwa katika taasisi
ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya
katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016). Kulia ni Mganga Mkuu wa
Taasisi hiyo, Dkt. Damian Msemo.
Na Beatrice Lyimo- Dar es salaam.
MAKAMU wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya
ziara yake ya kwanza katika Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuona wagonjwa sambamba na kuangalia maendeleo ya hospital hiyo.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Samia amebaini
baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ikiwemo ya upungufu wa
wauguzi na madaktari, uhaba wa mashine za mionzi, upungufu wa vifaa tiba pamoja
na upatikanaji wa dawa za Saratani kwa wagonjwa hao.
Amesema kuwa Serikali itahakikisha inaongeza
mashine mbili mpya za mionzi kwa ajili ya kupimia wagonjwa wanaosumbuliwa na
matatizo ya Saratani na kuahidi kupunguza deni la MSD wanaloidai hospital hiyo
ili wagonjwa waweze kupata dawa kwa gharama nafuu.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Damian Msemo ameiomba Serikali kuwekeza bajeti ya
kutoshakatika hospital hiyo kwani inatoa huduma bure kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa na matatizo hayo ambapo matibabu yake haa kwa upande wa mashine
ya mionzi hutumia gharama kubwa
Akifafanua utaratibu wa kutibu wagonjwa
wanaofika hospitalini hapo kutibiwa amesema kuwa hospitali hiyo imeweka
utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa hao ambapo mgonjwa anayefika mapema
ndiye anayehudumiwa na kuongeza kuwa
huwa wanatimu wagonjwa 160 kwa siku kuanzia asubuhi hadi usiku licha ya uhaba
wa vifaa tiba walionao”
“Hospitali hii tumeweka utaratibu mzuri wa
kuwahudumia wagonjwa wanaofika, mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa kwanza
ukiacha wagonjwa wa dharula” Amesema Dk. Msemo.
Amesema wagonjwa wanaowafikia kutibiwa
hospitalini hapo ni wengi ikilinganishwa na vifaa tiba walivyonanvyo na
kuwataka wananchi kuwa wavumilivu pale wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
Kwa upende wao baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata
matibabu wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taasisi hiyo kwa kujituma mbali
na uhaba wa waauguzi na changamoto za upatikanaji wa mashine za mionzi na dawa
kwa ajili ya kutibu matatizo hayo.
No comments:
Post a Comment