Mabadiliko
hayo yametangazwa na Meneja Uhusiano wa TRL Midladjy Maez wakati akizungumza na
waandishi wa habari Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Maez
amesema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya
huduma za Jiji kutoka kituo Kikuu cha Reli cha Dar es Salaam kwenda Pugu ambayo
itaanza kutoa huduma mapema siku ya Jumatatu ya tarehe 01/08/2016.
Aliongeza
kuwa mabadiliko hayo yanahusu treni za abiria za huduma za kawaida zinazoondoka
siku za Jumanne na Ijuma na kubainisha kuwa kwa upande wa huduma za treni ya
Deluxe zitaendelea na muda wake wa kawaida.
“Uongozi
umeamua kufanya mabadiliko haya kwa sababu za kiusalama zaidi kwani mabadiliko
haya yataepusha muingiliano unaoweza kupelekea ajali na kuongeza kuwa kwa safari za kutoka Kigoma na Mwanza muda umebaki uleule”. Alisema Maez.
Meneja
Uhusiano huyo aliongeza kuwa huduma za treni ya Jiji kwenda Pugu itakuwa na
vituo 10 ambavyoa alivitaja kuwa ni pamoja na Pugu Stesheni, Gongo la Mboto,FFU
Mombasa, Banana, (njia panda kwenda Stesheni), na karakata.
Vingine
ni pamoja na Vingunguti Mbuzi,SS Bhakressa, Kamata na Kituo Kikuu cha reli Dar
es Salaam.
Aliongeza
kuwa huduma hiyo itakuwa na awamu mbili asubuhi na Alasiri ambapo treni ya kwanza
itaondoka kituo cha Pugu saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es Salaam sa
12:55 asubuhi na kufanya safari tatu zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi.
Jioni kutakuwa na safari tatu ambapo treni itaondoka kituo cha Dar es Salaam saa 09:55 alasiri kwenda Pugu na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kuja Kituo Kikuu cha Dar es Salaam saa 03:20 usiku.
Jioni kutakuwa na safari tatu ambapo treni itaondoka kituo cha Dar es Salaam saa 09:55 alasiri kwenda Pugu na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kuja Kituo Kikuu cha Dar es Salaam saa 03:20 usiku.

No comments:
Post a Comment