Trending News

CCM Adverts and Promo

Wednesday, July 13, 2016

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AGAWA MADAWATI 61,385 LEO JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao ambapo pamoja na kuishukuru ofisi ya Bunge kwa kazi hiyo pia ameahidi serikali yake kuendelea kukabiliana na changamoto zilizokatika sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia. Leo katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao ambapo alisema ofisi ya bunge inatarajia kugawa jumla ya madawati 61,385 katika majimbo 155 kati ya majimbo 264 ambapo ni sawa na asilimia 59 wa madawati 120,000 yanayotarajiwa kutengenezwa na ofisi hiyo Leo katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mstahiki Meya Isaya Mwita akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya watoto wa shule ya msingi Bunge wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao, Leo katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua madawati katika mfano wa Darasa wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao, katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam. Anayemfuata ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh. Idd Azzan Madawati yaliyotolewa na Ofisi ya bunge kwa ajili kwa niaba ya wabunge waliopata mgao huo katika awamu ya kwanza.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao, katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka shule ya msingi Bunge iliyopo Jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Diwani, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mstahiki Meya Isaya Mwita na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.


(PICHA NA HASSAN SILAYO)



Na: Lilian Lundo 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya Usalama vilivyopewa jukumu la kutengeneza madawati kujipanga zaidi ili kutekeleza kwa wakati majukumu wanayopewa.

Mhe. Rais aliitoa kauli hiyo leo, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji wa madawati yaliyotolewa na Ofisi ya Bunge kwa Majimbo 155 ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawaji wa madawati hayo.

Mnamo april 11, 2016 Mhe. Rais alipokea hundi ya shilingi Bilioni Sita kutoka Ofisi ya Bunge na kuagiza fedha hizo zielekezwe katika utekelezaji wa utengenezaji wa madawati ambapo Magereza na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) walipewa jukumu la kutengeneza madawati hayo. 

Aidha Mhe. Rais amesikitishwa na kasi ambayo JKT na Magereza wametumia katika utengenezaji wa madawati hayo, ambapo kwa miezi mitatu wametengeneza jumla ya  madawati elfu Sitini.

“Nina wasiwasi na kasi yenu, ikiwa kwa miezi mitatu mmetengeneza madawati elfu sitini basi kuna uwezekano wa zoezi hili la utengenezaji wa madawati mkamaliza mwaka 2017,” alifafanua Mhe. Rais.

Aliendelea kwa kusema kuwa, suala la madawati ni la haraka alihitaji kusubiri kwa muda mrefu hivyo vyombo hivyo vinatakiwa kutengeneza madawati hayo kwa uharaka kwani nguvu kazi ya kutosha wanayo.

Kwa upande wake, Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa Ofisi ya Bunge inategemea kugawa madawati 120,000 kwa awamu mbili tofauti ambapo awamu ya kwanza imekamilika na jumla ya madawati 61,385 yatagawiwa kwa majimbo 155 kati ya majimbo 264.  

Fedha iliyotolewa na Ofisi ya Bunge ni Fedha iliyotokana na matunda ya  mpango wa Serikali wa kubana matumizi ambapo Ofisi ya Bunge imeweza kubana matumizi na kubaki na Shilingi Bilioni Sita kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

No comments:

Post a Comment