Trending News

CCM Adverts and Promo

Tuesday, July 12, 2016

WAKURUGENZI WAPYA WAAPISHWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AWATAKA KUSHUGHULIKIA KERO ZA WANANCHI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuwatumikia wananchi ikiwemo kuondoa kero zinazowakili wananchi katika maeneo yao kama utitiri wa kodi hasa kwenye bidhaa wanazozalisha.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya (Hawapo pichani) walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kwenye matumizi ya Kanuni, Sheria na Taratibu katika kutimiza majukumu yao. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim akiongea na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa dhumuni la kuwaletea wananchi maendeleo.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Maadili Kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akiongea akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kuzingatia maadili katika kipindi chao cha uongozi wakati wa hafla ya uapishwa wa kiapo cha Ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi hao.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.  


Kamishna wa Maadili Kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akiongea akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kuzingatia maadili katika kipindi chao cha uongozi wakati wa hafla ya uapishwa wa kiapo cha Ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi hao.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma na kuwataka kuepuka vishawishi ikiwemo kupokea rushwa. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni wakila kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Luhende Pius akionesha cheti chake cha taalum kwa waandishi wa habari baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na uwepo wa taarifa potofu juu ya taaluma yake. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya aliowateua hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Bw. Elias Nawela. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Picha na Hassan Silayo 

Na Jonas Kamaleki - Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmshauri zote nchini kuondoa kero za wananchi na si kuwaongezea kero.

Hayo ameyasema leo kwenye hafla ya Kiapo cha Uadilifu wa Utumishi wa umma kwa Wakurugenzi Watendaji wa Majiji, Manispaa, Miji na Halmashauri nchini,iliyofanyika Ikulu jijini  Dar es Salaam.

“Anzisheni miradi inayotatua kero za wananchi na si kuwaongezea kero, kila eneo lina kero zake hivyo jitahidini kuziondoa,”alisema Rais Magufuli.

Amewataka Wakurugenzi hao kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wananchi kwani wamechoshwa na kero hasa kwenye ushuru na kodi zisizo za lazima, akitolea mfano mkulima wa mchicha na mpunga kutozwa kodi wakati amelima kwa ajili ya chakula chake ya kwamba hili jambo halikubaliki.

Rais Magufuli amewaambia Wakurugenzi kuwa anawaamini kwani uteuzi wao ulifanywa kwa umakini na akaonyeshwa kushangazwa na waliokuwa wakibeza uteuzi huo hasa waliosema kuwa amemteua mwenye cheti cha usimamizi wa hoteli.

“Majina kufanana si tatizo, mimi niliyemteu ni Bwana Luhende ambaye ana diploma na masters (shada ya uzamili), Bwana Luhende hebu simama wakuone na vyeti vyako,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa hakubahatisha katika kuteua Wakurugenzi hao na kuongeza kuwa kazi hiyo ameifanya kwa umakini mkubwa.

Rais amewataka Wakurugenzi kuhakikisha wanakusanya na kusimamia kodi za wananchi ili kuwaletea maendeleo na kuwaondolea matatizo ambayo yamewachosha.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan amewataka Wakurugenzi kuwa watumishi wa watu na si watawala.

Amewaasa Watendaji hao kujifunza sheria na kanuni zinazohusiana na kazi zao na kuwataka wawe waadilifu na wachapakazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Naye Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majali Majaliwa amewataka Wakurugenzi kuwa wawajibikaji, waadilifu na waaminifu.

“Ninyi ni injini ya maendeleo katika nchi kupitia kwenye Halmashauri zenu na kazi yenu kubwa ni kusimamia watumishi katika kuleta maendeleo katika sehemu zenu,”alisema Majaliwa.

Amewataka Wakurugenzi kukusanya kodi na kuzitumia katika miradi ya maendeleo kwa uaminifu na kuwasisistiza kuzingatia thamani ya fedha katika mradi husika (Value for Money)

Jumla ya Wakurugenzi 185 wamekula kiapo cha uadilifu katika utumishi wa umma na kuhudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

No comments:

Post a Comment