Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
HMwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wakiwa tayari meza kuu kuendesha kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, mtarajiwa Rais Dk John Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na kulia niMakamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Wajumbe wa NEC wakiwa wamenyoosha mikono kushirikia kulipitisha jina la Rais Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM, kufuatia kulipitisha, jina hilo kesho litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ili kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.



No comments:
Post a Comment