JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Agosti, 2016 amepokea
taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi
asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga
Mkoani Lindi.
Mwakilishi Mkazi
wa Kampuni ya Statoil ya nchini Norway ambayo ni moja ya Kampuni zitakazowekeza
katika mradi huo Bw. Oystein Michelsen amemueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa
kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Bilioni 30 sawa na zaidi
ya Shilingi Trilion 65 za Kitanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua
muda wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.
Bw. Oystein Michelsen
amebainisha kuwa Serikali ya Norway ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mradi
huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na ameomba Serikali ya Tanzania
iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.
Kwa upande wake
Rais Magufuli amemuhakikishia Mwakilishi huyo wa kampuni ya Statoil kuwa
Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi unafanikiwa na ameitaka
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
kushirikiana na wadau kutoka Wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa
ujenzi wa kiwanda hicho.
"Nataka kuona
mradi huu unaanza kujengwa, tunachukua muda mrefu mno, kamilisheni mambo
yaliyobaki ili wawekezaji waanze kazi mara moja"
Amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli
amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira kwa idadi kubwa ya watanzania na
utaiwezesha serikali kupata mapato kupitia tozo mbalimbali, na hivyo kutumika
kuimaisha huduma za kijamii zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu.
Pamoja na Statoil
kampuni nyingine zinazoshiriki katika uwekezaji wa mradi huu ni Shell, Exxon
Mobil, Pavillion na Ophir.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
Salaam
22 Agosti,
2016
No comments:
Post a Comment