Naibu Balozi wa China nchini Bw.Gou Haodong akizungumza
jambo na wanafunzi wa kitanzania waliopata ufadhili wa kwenda China kusoma
masuala ya mafuta na Gesi leo jijini Dar es Salaam.
Habari/Picha na Daudi Manongi
WAZIRI
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter
Muhongo amekabidhi nyaraka za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 20 wa kitanzania
wanaokwenda kusoma fani za mafuta na gesi katika ngazi za uzamili na uzamivu
nchini China.
Watanzania
hao 20 wamepatikana kutokana na mchujo na Wizara hiyo ukihusisha watanzania 89 kwenye
ngazi mbalimbali za elimu nchini.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi nyaraka hizo leo Jijini Dar es Salaam, Prof. Muhongo
alisema kuwa wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikisomesha vijana wa
kitanzania nje ya nchi kwa ajili ya kusomea masuala ya mafuta na gesi.
“Serikali
ya China imetoa nafasi kwa vijana wa kitanzania kusoma nchini mwao na kwa jinsi
ilivyo tukaona ni vyema tuzitangaze nafasi hizi kwa Watanzania wote kupitia
wizara yetu ili waweze kuisaidia nchi yao na baada ya mchujo leo hii
tunawakabidhi nyaraka zao za masomo” alisema Profesa Muhongo.
Aidha
Profesa Muhongo aliwataka vijana hao kuitumia vyema nafasi waliyoipata na
kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwani nchi inahitaji wataalamu wa kutosha katika
sekta ya mafuta na gesi ambayo inakua kwa kasi ya haraka nchini.
Kwa
upande wake Naibu Balozi wa China Nchini Bw.Gou Haodong amewaasa watanzania hao
kusoma kwa bidii wakiwa nchini china na kuhakikisha wanafikia malengo yao ya
kitaaluma.
Pia
amewaasa kuhakikisha wanawafundisha watu wa china utamaduni wa mtanzania na
wawe mabalozi wazuri wa nchi yao.
Serikali
ya China inatoa ufadhili wa nafasi 20 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitano
kwa watanzania ili kujifunza masuala ya Gesi na Mafuta nchini mwao kupitia Wizara
ya nishati na madini.
|
No comments:
Post a Comment