Trending News

CCM Adverts and Promo

Monday, August 29, 2016

WAZIRI MAKAME MBARAWA: LENGO LETU NI KUYABADILI MAISHA YA WATANZANIA KUPITIA MIUNDOMBINU.

Akizungumza katika TUNATEKELEZA TBC1 leo hii Prof Makame Mbarawa ameainisha masuala muhimu ya kiutekelezaji katika wizara yake kama ifuatavyo:-
 #Prof Mbarawa: Rais Magufuli amedhamiria kuleta HapaKaziTu ya kweli katika sekta ya miundombinu;

 #Prof Mbarawa: Sekta hii imetengewa zaidi ya Sh. Trilioni 4 ambapo Bil 500 ni maalum kwa ajili ya kufufua Shirika la Ndege;

 #Prof Mbarawa: Tumeanza kutekeleza ahadi ya kuwapatia meli kubwa na ya kisasa Ziwa Victoria.Tenda inafunguliwa;

#Prof Mbarawa: Reli ya kiwango cha Standard gauge itajengwa kwa mtindo wa wakandarasi tofauti ili imalizike haraka;

#Prof Mbarawa: Tutaboresha eneo na kivuko cha Kigamboni? Ukarabati wa vivuko unakamilika..tozo za daraja tumepokea maoni mapya ya wadau tutayafanyiakazi;

#Prof Mbarawa; Shirika letu la ndege ni kama lilikuwa limekufa..sasa tunalifufua; #Prof Mbarawa: Ndege mbili mpya za kwanza aina ya Bombadier Q400 zitawasili Dar Sept. 19, 2016;

#Prof Mbarawa; Tumenunua ndege hizi zenye usalama mkubwa, uwezo wa kutua popote nchini hata kwenye viwanja vyenye changarawe tu au vyenye eneo dogo tofauti na ndege nyingine na zinatumia mafuta kidogo sana;

#Prof Mbarawa: Kwa kununua moja kwa moja kwa watengenezaji tumetumia USD mil. 23.5 kwa kila moja wakati bei ya sokoni ni USD mil. 31 kwa ndege moja;

#Prof Mbarawa: Tumeanza kuboresha viwanja vya ndege Dodoma, Mwanza, Kigoma na kwingineko. Lengo ni mikoa yote nchini kuwa na viwanja vya ndege vyenye kiwango cha lami ndani ya miaka minne ijayo;

#Prof Mbarawa: Kuhusu Bandari tunaendelea kuboresha ushindani wa kibiashara na kuongeza mapato;

#Prof Mbarawa: Nimeagiza wafanyakazi wote wa Bandari waliohusika kufunga mifumo ya chini ya kiwango ya TEHAMA huko nyuma wachukuliwe hatua;

 #Prof Mbarawa; Nimeipa Bodi ya Bandari lengo la kukusanya Sh. Trilioni 1 mwaka huu wakishindwa bila sababu nitawaonesha mlango wa kutokea;

#Prof Mbarawa: Tunakwenda kuifanya kampuni ya simu nchini kuwa bora zaidi.Tumeshawalipa Airtel hisa zao sasa tunaimiliki TTCL kwa asilimia 100;

 #Prof Mbarawa: Tuliwatengea ruzuku makampuni ya simu kuweka minara ya simu mikoani wakashindwa kutekeleza...tumeleta Viatel wamejenga mtandao mkubwa na sasa mawasiliano ya simu vijijini yamekuwa bora zaidi nchini

Prof Mbarawa: Nia yetu ni kuifanya sekta ya miundombinu na mawasiliano kuwa chachu ya kuifikia Tanzania ya viwanda.

No comments:

Post a Comment