Mhe. Hamad Masauni -Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Serikali
imeiagiza Idara ya Uhamiaji kuhakikisha inasimamia sheria kwa kuyakamata na
kuyataifisha magari yote yanayotumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka nje
ya nchi.
Pia,
serikali imewaonya wanaojihusisha na mtandao wa kusafirisha wahamiaji haramu
kuacha mara moja na kutafuta kazi nyingine za kufanya kwani serikali iko makini
kudhibiti wahamiaji haramu.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni,
alipotembelea mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga mwishoni mwa wiki, ili
kujionea changamoto zilizopo mpakani na kuelewa hali halisi.
Masauni
amewatahadharisha watumishi wa Idara hiyo kuwa endapo gari litakamatwa katika
eneo lolote nchini likiwa na wahamiaji haramu kupitia mpaka huo, watakuwa wameidanganya
Serikali na kuidhihirishia kuwa majukumu yao yatakuwa yamewashinda.
Amesema
pamoja na kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na idara hiyo ya uhamiaji
Namanga kudhibiti wahamiaji haramu, bado zipo njia za panya zinazotumiwa na
wahamiaji hao mmoja mmoja kwa kushirikiana na Watanzania wachache wanaofanya
kazi ya kuwavusha kwa kulipwa ujira kinyume cha sheria.
Ameitaka
idara hiyo kutumia vitendea kazi vichache ilivyonavyo pamoja na waumishi
wachache waliopo ili kudhibiti mianya inayotumiwa na wahamiaji hao. Pia,
aliagiza doria za mara kwa mara na kuimarisha ukaguzi ndani ya magari ili
kubaini wahamiaji haramu.
Alisema
idara hiyo inafanya kazi kwenye mazingira magumu kutokana na uhaba wa vitendea
kazi, ukubwa wa eneo la mpaka hivyo akatoa wito kwa wananchi kusaidia
kuwafichua wahamiaji haramu.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amesema idara hiyo inakabiliwa na
changamoto zilizopo mpakani hapo kutokana na ukubwa wa eneo la mpaka hivyo
inashindwa kudhibiti eneo hilo kikamilifu.
Awali,
Mkuu wa idara hiyo katika eneo hilo la Namanga, Abdalah Katimba, alisema
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo upungufu wa watumishi na
vitendea kazi.
No comments:
Post a Comment