Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea msaada wa fedha kiasi cha dola laki mbili (USD 200,000) kutoka
kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka
(kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda
Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi Mkoani
Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface Muhia mara baada
ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na
kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka
Kenya muda wowote
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa
kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
mchango wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000)
uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya
kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili
(USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha/IKULU.
No comments:
Post a Comment