Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani
akiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, Butiama Musoma akiwa ameambatana na watumishi wa NEC na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT
kutoka maeneo mbalimbali kuzuru kaburi
la Baba wa Taifa, Mwitongo wilayani Butiama. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iko
mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
Muongoza
wageni wa maeneo ya historia nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwitongo Butiama Bi.
Gaudensia Waziri akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima
Ramadhani (mwenye kofia) kuhusu Kaburi na historia ya Chifu Burito aliyekuwa chiefu
wa Kabila la Wazanaki.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani (Kushoto)
akisalimiana na Msemaji Mkuu na kiongozi wa familia ya Baba wa Taifa Chifu
Japhet Wanzagi (kulia) mara baada ya kuwasili eneo la Mwitongo wilayani
Butiama. Wa Pili kutoka Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi. Annarose
Nyamubi.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasha
mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la
Mwitongo, Butiama. Wengine wanaoonekana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT
na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mwongoza
wageni na Mhifadhi wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama, Jacob Thomas akitoa
maelezo kuhusu picha za kumbukumbu za Baba wa Taifa kwa Mkurugenzi wa NEC Bw.
Kailima Ramadhani na watumishi wa NEC walioitembelea makumbusho hiyo eneo la
Mwitongo, Butiama –Musoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NEC
waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mwitongo, Butiama.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi waandishi wa habari wa mkoa
wa Mara waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere Mwitongo, Butiama. Watendaji wa NEC wako mkoani Mara kutoa elimu ya
mpiga kura kwa wananchi.
Na. Aron Msigwa –
NEC, Musoma.
Viongozi wa vyama vya
Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili
kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa
na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima
Ramadhani mara baada kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.
Amesema kuwa kumbukumbu
za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi
ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia
wananchi.
“Kupitia kumbukumbu
hizi sisi watumishi wa Tume tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao
Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika, wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa
uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema
Kailima.
Ameeleza kuwa maisha
aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa
pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka
na mali kwa manufaa ya taifa.
“Sote ni mashahidi
kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu Nyerere kabla
hajajengewa nyumba na Jeshi, kama Rais
mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika
eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa
mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Kailima.
Bw. Kailima amebainisha
kuwa NEC itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya
na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na
waridhike na vile walivyonavyo.
“Suala la kuridhika na
kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa
wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,
matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi
wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”
Ameainisha Kailima.
Kwa upande wake
Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw.
Jacob Thomas amesema kuwa watanzania
wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo
vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.
Amesema kuwa maisha
ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea
maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na
viongozi wa Tanzania.
“Ninyi mliopata nafasi
ya kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na
dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania”
No comments:
Post a Comment