Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Rais mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Hongera!!
Umekiongoza chama chetu kwa mafanikio
ukitumia Hekima, Busara na maarifa kuhakikisha kuwa chama chetu kinakuwa imara
na kinaendelea kushika dola na kuongoza Serikali. Imani waliyoijenga watanzania
kwa Chama chetu na kukipa ushindi wa kishindo katika Chaguzi zote ni
kielelezo cha uongozi wako uliotukuka.
Umetuachia Chama imara na Serikali imara
yenye uwezo wa kusimamia maendeleo ya Nchi yetu.
Katika kipindi chote cha uongozi wako
umehakikisha kuwa Chama na Jumuiya zake kimeendelea kuwa Imara na hususani
Jumuiya ya Wazazi ambayo bila miongozo yako isingekuwa hivi ilivyo leo.
Umetujengea imani ndani ya Jumuiya na ndani ya Chama na kutufanya tujisikie ni
sehemu muhimu ya Chama chetu. Tutaendelea kukuenzi ndani ya Jumuiya na Chama
chetu kwa ujumla.
Umoja wa Wazazi, Jumuiya ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kwa heshima na unyenyekevu mkubwa unapenda
kukupongeza Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kuliongoza Taifa letu kwa kipindi cha miaka 10.
Tunatambua ukuu na ugumu wa kazi hii
kubwa kuliko zote nchini mwetu na tunazielewa changamoto nyingi ulizokumbana
nazo katika kipindi chote cha miaka 10. Tunafahamu mzigo wa kutekeleza
matumaini na matarajio ya kila mtanzania kwa kipindi cha miaka 10. Kwa kutambua
yote haya na kwa kutambua jinsi ulivyoifanya kazi hii kwa uadilifu uzalendo na
umakini wa hali ya juu, tuna kila sababu ya kukupongeza na kukushukuru kwa
jinsi ulivyojitolea kulitumikia Taifa lako.
Mhe. Rais, umefanya mambo mengi
katika kipindi cha uongozi wako na kwa heshima sisi Umoja wa Wazazi, Jumuiya ya
CCM Mkoa wa Morogoro tunaomba tuyakumbuke na kuyataja machache kwani kwa nafasi
ya makala hii pekee haitatosha kuyaeleza yote.
Mhe. Rais kwanza kabisa tunakupongeza
na kukushukuru kwa kuenzi na kusimamia Amani, Umoja na Mshikamano wa Watanzania.
Tunatambua kuwa hii ilikuwa ajenda yako ya kwanza na hakika tunakushukuru kwa
kulinda na kuitunza tunu hii muhimu kwa Taifa letu.
Mhe. Rais, Amani na utulivu ndio
msingi wa uimara wa Taifa lolote, tunatambua jinsi ambavyo umesimamia na
kulinda na ushuhuda wa hili ni jinsi ambavyo umekuwa mstari wa mbele kuihubiri
kwa maeneo na vitendo. Ahsante Mhe. Kikwete kwa kuiacha nchi ikiwa tulivu na
salama.
Jambo la pili Mhe. Rais ni juhudi na
mchango wako katika kukuza na kusimamia Demokrasia nchini mwetu. Katika kipindi
cha uongozi wako tumeshuhudia demeokrasia ikipanuka na uhuru wa vyombo vya habari
na watu kujieleza umepanuka zaidi., vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya Jamii
yamepata fursa ya kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi pengine kuliko kipindi
chochote tangu tupate uhuru.
Busara, hekima na utashi wako wa
kutaka kila mtu asikike ndio msingi wa kukua na kuimarika na hata wenzetu wa
upande wa pili ni mashuhuda wa hili japokuwa mwanadamu ameumbwa kutoridhika
hawawezi kuacha kupiga kelele kwa hili pia Mhe. Rais tunaomba tukushukuru.
Jambo la tatu mhe. Rais ambalo
Mtanzania yeyote muungwana hawezi kukusahau ni uimarishaji wa miundombinu
hususani barabara.
Taifa letu halijawahi kushuhudia
barabara bora za kiwango cha lami kwa urefu tulionao sasa. Tunafahamu kuwa,
hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo ya haraka na hata kukua kiuchumi kama
hakuna miundombinu imara ya usafirishaji. Leo hii kila kona ya Tanzania
inafikika kwa mchana mmoja na thamani ya mazao inaongezeka kwani kuna unyumbafu
wa kutosha wa biashara ya mazao ya kilimo na biashara.
Hata wanaobeza mafanikio yako mioyoni
wanasutwa na mafanikio uliyoyapata kwenye sekta ya uchukuzi, kwani kwa sasa
kila mkoa umeunganishwa na barabara za lami.
Jambo la nne Mhe. Rais ni mchango
wako na kujitoa kwako katika kuimarisha elimu. Umefanya mengi na kila mwenye
nacho ni shuhuda, wapo wanaotamba kuna wao ndio waliojenga shule za kata na
chuo kikuu cha Dodoma. Hiki ni kichekesho . Mafanikio yote haya yamekuja chini
ya uongozi wako tumepata shule za kata, tumepata shule za msingi tumejenga
maabara za kutosha kila shule na tumepata chuo kikuu cha Dodoma ambacho ni
kikubwa kuliko chuo chochote Afrika Mashariki. Mafanikio haya si madogo na hayakushuka kama maua jangwani bali
yametokana na uongozi wako mahiri na mapenzi uliyonayo kwa nchi yako na
watanzania wanzeko.
Jambo la tano ambalo Mhe. Rais
tunapenda kukupongeza ni uimarishaji wa Sekta ya Afya. Tunashuhudia ukihakikisha
kuwa hospitali nyingi zinapanda hadhi na kuwa hospitali za Wilaya na za Rufaa.
Dhamira yako ya kusogeza huduma bora za afya karibu na wanachi zimezaa matunda na leo
tumeshuhudia upasuaji mkubwa wa moyo ukifanyika katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.
Tunaomba Rais ajaye ambaye tunaamini atatoka CCM, aanzie ulipoishia kwa
kuendelea kusogeza huduma karibu na wanachi, kuongeza watumishi pamoja na
kuhakikisha madawa yanapatikana.
Jambo la sita Mhe. Rias ni sekta ya
michezo. Umefanya makubwa na yoote uliyoahidi ikiwemo kulipia gharama za
wataalamu na wakufunzi umeyatimiza. Umekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki
za wasanii na hata kusaidia ukuaji wa tasnia ya sanaa na muziki, Tanzania
vinajiendesha kibiashara vinaleta ajira na kuwapatia wasanii vipato vya jasho
lao.
Jambo la saba Mhe. Rais ni fursa kwa
wanawake. Wewe ni muhimili mkubwa wa fulsa ya “Wanawake Wanaweza” umefanya
makubwa kwa kuwawezesha na kuwainua akina mama ikiwemo kuongeza idadi yao
katika nyadhifa za kuchaguliwa na kuteuliwa. Leo hii tumeshuhudia akina mama
wakishiriki katika ujenzi wa Taifa, wapo Mawaziri, Makatibu wakuu, Wakurugenzi,
Majaji, mahakimu, Wabunge, wawakilishi na hata Spika wa bunge lililomaliza muda
wake ni mwanamke. Tumekupongeza kwa ujasiri wa kuwaamini kina mama na hakika
hawakukuangusha.
Jambo la nane Mhe. Rais ni mchakato
wa Katiba. Ulithubutu na ukaweza kuanzisha na kusimmia mchakato wa Katiba kwa
mara ya kwanza tangu awamu ya kwanza umefanya uamuzi mgumu na wa muhimu wa
kuanzisha mchakato wa Katiba . Ni matumaini yetu kuwa Raisi ajaye kutoka CCM
atakaribisha mchakato na kutupatia katiba bora kwa ajili ya maendelezo ya Taifa
letu.
Mhe. Rais umefanya mengi lakini kama
ilivyo hapo awali tumetaja machache.
Itoshe tu kusema asante sana kwa utumishi uliotukuka. Daima tutakukumbuka na
kuyaenzi mafanikio yako. Tunakupongeza sana sana. Mama yetu mama Salma na
familia yako kwa kukubali kukuachia uwatumikie watanaznia kwa moyo mmoja.
Tunajua waliku- miss na sasa ni wakati wako wa kupumzika na kuungana na familia
yako.
Mungu akujalie afya njema katika
kipindi chote cha mapumziko na tunaomba uache milango wazi tuendelee kuchota
burasa zako.
AHSANTE BABA KIKWETE!!!!!!

No comments:
Post a Comment