Trending News

CCM Adverts and Promo

Sunday, December 13, 2015

SALAAM ZA PONGEZI KWA RAIS.DKT.J.P MAGUFURI KUTOKA JUMUIYA YA WAZAZI CCM-MOROGORO


KARIBU DKT.JOHN P. MAGUFULI, tuchape kazi uchaguzi umekwisha na wananchi wameongea na sauti zao zimesikika kupitia masanduku ya kura. Ni dhairi kuwa Dkt. John Pombe Magufuli ndiye Rais wa  awamu ya tano wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya umoja wa Wazazi, Jumuiya ya CCM Mkoa wa Morogoro tumependa kukupongeza wewe binafsi, Viongozi na wanachama wote wa chama cha Mapinduzi  kwa ushindi mkubwa tulioupata . Ushindi huu unaonyesha kuwa wananchi wana imani na wewe lakini pia bado wana Imani na chama chetu cha Mapinduzi.

Lakini kama Jumuiya tumependa pia kuwapongeza wabunge wote wa Mkoa  wa Morogoro na Nchi nzima kwa ujumla kwa kushinda na kuchaguliwa  kuwawakilisha wananchi kwenye baraza hilo muhimu la kutunga sheria. Uchaguzi  umekwisha ni wakati wetu sote kumsaidia Rais wetu kutekeleza majukumu yake bila kujali itikadi zetu kwani kama ambavyo mhe. Rais amekuwa anasema  “maendeleo hayana vyama”.

Mhe.Rais,Dkt.John Pombe Magufuri akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazizi Mkoa wa Morogoro,Bi.Mecky Mdaku

Mhe. Rais , Sisi Wazazi Morogoro  tunakukaribisha na tunaahidi ushirikiano wetu kwako katika kusimamia shughuli za Serikali na chama chetu. Matarajio ya Watanzania kwako ni makubwa nasi tunaimani kuwa kwa uwezo na moyo ulionao wa kuwatumikia Watanzania na kwa msaada wa Mungu ambaye amekuwa nguzo yako kuu utafanikiwa.

Mhe. Rais Ilani  ya chama chetu imefafanua vizuri vipaumbele na namna ambavyo tumejipanga  kutatua kero za Watanzania na kuboresha maisha yao. Katika kipindi cha kampeni umefanya kazi kubwa ya kuinadi  na kuifafanua Ilani yetu na huu ndio msingi wa ushindi wetu kwani tunayaamini watanzania walikuelewa na kukuamini.

Ulipita kila kona ya nchi hii tena kwa usafiri wa barabara jambo ambalo si  tu lilikupa fursa ya kuwafikia watanzania wengi, bali pia ulipata fursa ya kushuhudia changamoto wanazokabiliana nazo.

Tunapenda kukupongeza wewe na timu nzima ya Kampeni akiwemo Mwenyekiti wetu wa Umoja wa Wazazi, Jumuiya ya CCM Tanzania Abdallah M.Bulembo kwa kazi kubwa mliyoifanya.
 Mhe. Rais dhamira tuliyopewa na wananchi ni kubwa na Imani waliyoonyesha kwetu haina kipimo. Tunalo deni kwa watanzania  na kama ulivyokwisha sema inatubidi tufanye kazi , tunapenda kukuunga mkono na kuwaomba viongozi wote watakaoteuliwa na watanzania kwa ujumla wajiandae kuchapa kazi kwa bidii.

Uwezo wako na dhamira yako haitiliwi shaka na mtu yeyote hivyo tunaimani kuwa ahadi tulizowapa watanzania tutazitekeleza kwa uongozi wako. Uwezo wa kuondoa kero za watanzania unao, uwezo wa kuongeza ajira kwa vijana unao, uwezo wa kusimamia rasilimali za Taifa unao, uwezo wa kusimamia misingi ya haki na Amani ya nchi yetu unao, Uwezo wa kusimamia umoja na mshikamano ndani ya chama chetu na Serikali zake unao. Lakini kikubwa kabisa ni kuwa nia na dhamira ya dhati ya kuwatumiakia wananchi unayo.

Kwa mtaji huu Tanzania yenye uchumi wa kati, yenye Viwanda na uwezo wa kutumia malighafi za ndani yenye kuboresha maisha ya wafanyakazi, wakulima  na  wafugaji ndio Tanzania ya Magufuli  tunayoingojea. Ukweli ni kuwa Tanzania ya aina  hii chini ya Uongozi wako inawezekana na kila mmoja atimize wajibu wake.   

Tuna Imani kuwa Serikali unayoenda kuiunda itakuwa na sura zinazofanana na wewe kiutendaji, itakuwa na watanzania wazalendo na wachapakazi na wenye uchungu na Taifa lao. Tunajua utaunda Serikali ya watu wanaochukia rushwa na kubwa Zaidi wanaochukia umaskini wa watanzania.
Kwa upande wa chama chetu huu ni wakati wa kutathimini yote yaliyyotokea kipindi cha kampeni. Upo ukweli kuwa baadhi ya wana CCM walishiriki kukihujumu chama kwa njia moja au nyingine. Wapo walioshindwa kutimiza majukumu yao kwa uzembe lakini wapo pia waliotuhujumu kwa kukusudia.

Sisi Jumuiya ya WAZAZI Morogoro tunaamini kuwa adui wa ndani ya chama ni hatari kuliko adui wa nje wa chama.

Tunakutakia Afya njema na maisha marefu ili uweze kutimiza ndoto  zako za kuboresha maisha ya watanzania. Karibu Dkt. John P. Magufuli.

Kidumu chama cha mapinduzi.

No comments:

Post a Comment