Trending News

CCM Adverts and Promo

Monday, April 11, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANNE KILANGO MALECELA

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela. Uamuzi huo umekuja baada ya Kilango kutoa taarifa ya uongo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa katika mkoa wake hakuna mfanyakazi hewa hata mmoja.

Kwa mujibu wa Rais, baada ya kupata taarifa hiyo aliitilia shaka kwa kuwa anaamini hakuna mkoa ambao hauna mfanyakazi hewa. Kutokana na taarifa hiyo ya Kilango, Rais aliamua kutuma kikosi kazi kuhakiki taarifa hiyo ndipo usiku wa kuamkia leo aliletewa taarifa ya awali iliyoonesha kuwa mkoa wa Shinyanga hadi sasa hivi una watumishi hewa 45 na ni matumaini ya Rais kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Pia Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga naye amefutwa kazi kutokana na kutoa taarifa hiyo ya uongo. Mpaka hapo, Anne Kilango Malecela amedumu katika utumishi wa umma kama mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa siku 28 tangu alipoapishwa tarehe 15 Machi 2016.


KUSIKILIZA HOTUBA YAKE BOFYA HAPO CHINI

No comments:

Post a Comment