Muonekano
wa Kivuko cha MV Tanga, kitakachotoa huduma ya usafirishaji katika Wilaya ya
Pangani mkoani Tanga ambacho ukarabati wake umekamilika tayari kwa kuanza kazi.
********************************************************************
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, amekagua na kuridhika
na hatua ya ujenzi na ukarabati wa vivuko vitatu na tishari moja unaoendelea
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kukagua ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, New MV
Magogoni na Tishari litakalotumiwa na Kivuko cha MV Dar es Salaam Eng.
Nyamhanga amewapongeza mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni
ya M/S Songoro Marine Transport Boat Yard Ltd kwa kufanya kazi kwa kasi na
ubora unaotakiwa.
“kazi
yenu ya ujenzi na ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, Kivuko kipya
cha Magogoni na Tishari inafanyika kwa viwango vinavyokubalika na hivyo baadae
mwezi huu, vivuko vya MV Tanga na MV Magogoni vitaanza kazi, Hongereni”,
amesema Eng. Nyamhanga.
Eng.
Nyamhanga amesisitiza nia ya Serikali kuhakikisha Ujenzi na Ukarabati wa vivuko
unafanyika hapa nchini ili kuzipa nguvu kampuni za kizalendo na kupunguza
gharama za utengenezaji na ukarabati nje ya Nchi.
Kukamilika
kwa Kivuko cha MV Magogoni chenye uwezo wa kubeba abiria 2000 na magari 60
kutapunguza msongamano katika kivuko cha Kigamboni na kuimarisha huduma ya
usafiri kati ya Kigamboni na Magogoni.
“Hakikisheni
ujenzi wa Tishari na Kivuko kipya cha Magogoni unakwenda kwa kasi, ili kukamilisha
mkakati wa Serikali wa kuhuisha usafiri wa majini hapa nchini.” Amesisitiza
Eng. Nyamhanga.
Naye
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan amemhakikishia Katibu Mkuu
sekta ya ujenzi kuwa, ushirikiano kati ya TEMESA na kampuni ya Songoro, katika
ujenzi na ukarabati wa Vivuko na Tishari ni mzuri na utakamilika kwa wakati.
Kukamilika
kwa Kivuko kipya cha Magogoni kunafanya TEMESA kuwa na vivuko 30 vinavyotoa
huduma katika maeneo mbalilmbali nchini kote.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
|
No comments:
Post a Comment