Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto)
akimsikiliza kwa makini Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu Dk. Stella Rwezaura
aliyekuwa akitoa maelezo kuhusu matibabu Bi. Kuluthumu Kasongo (aliyelala kitandani)
anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell) ili kujiridhisha juu ya
matibabu yake kufuatia taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii leo kuwa
mgonjwa huyo ametelekezwa bila kupatiwa matibabu na kulazwa chini katika wodi
hiyo jambo ambalo sio la kweli.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto)
akipitia kwa makini jalada (file) la matibabu Bi. Kuluthumu Kasongo (aliyelala
kitandani) anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell) kujiridhisha
juu ya matibabu yake kufuatia taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii
leo kuwa mgonjwa huyo ametelekezwa bila kupatiwa matibabu na kulazwa chini
katika wodi hiyo jambo ambalo sio la kweli.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kushoto)
akiwa ameongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi
kufuatilia ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo jijini Dar es salaam
kuangalia ubora wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali hiyo.
Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla (kulia) juu ya huduma za Tiba alipotembelea wodi ya watoto njiti
katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kulia)
akizungumza na akina mama wenye watoto waliokuwa katika wodi ya Wazazi ya
Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara
ya kushtukiza katika hospitali hiyo.Amewahakikishia akina mama hao kuwa
Serikali itaendelea kuboresha huduma za Afya katika hospitali zake.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia)
akimsalimia mtoto aliyekuwa amelala na akina mama wenye watoto aliowakuta
katika wodi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es
salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo kukagua
ubora wa huduma za Afya.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia)
akiwa nje ya Jengo la Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T)
LIMITED mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufuatia mmiliki wa kituo
hicho Tabibu Juma Mwaka kuendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa siri pia
kujitangaza kwenye vyombo vya habari licha ya agizo la Serikali la Julai 11,
2016 la kumtaka asitishe kutoa huduma zake kutokana na kukosa vigezo vya
kisheria vya kumruhusu kutoa tiba nchini.
Baadhi ya Wagonjwa waliokutwa
wakisubiri Tiba katika kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN
(T) LIMITED kilichopigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla
(kulia) akizungumzwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Tiba
Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED waliokuwa wakitoa huduma licha
ya kituo hicho kupigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.Kufuatia
hali hiyo Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi
kumkamata ndani ya saa 24 na kumfikisha Mahakamani Mmiliki wa Kituo hicho
tabibu Juma Mwaka kwa kukiuka agizo la Serikali na kutoa huduma kinyume cha
Sheria.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia),
Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba
Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) kwa pamoja
wakipitia kwa makini baadhi ya nyaraka zilizokutwa ndani ya kituo cha
Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala
Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar
es salaam kwa lengo la kuchukua vielelezo kama ushahidi wa Tabibu
Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia),
Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba
Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) kwa pamoja
wakipitia kwa makini baadhi ya nyaraka zilizokutwa ndani ya kituo cha
Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala
Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar
es salaam kwa lengo la kuchukua vielelezo kama ushahidi wa Tabibu
Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria.
Baadhi ya Dawa zilizokutwa zikitumika katika
kituo hicho ambazo nyingine zimemalizika muda wake wamatumizi toka Machi, 2015.
Daftari la lenye orodha
ya mahudhurio ya wagonjwa lililokutwa dani ya kituo cha Tiba Asili na
Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi
uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia)
akiongea na waandishi na wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa
Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia
hatua kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba Asili na Tiba
Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria. Picha/ARON MSIGWA -MAELEZO.













No comments:
Post a Comment