Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya
Ushauri TFDA wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
Habari/Picha Na Ally Daud - Dar es salaam.
Serikali imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za
binadamu katika viwanda vya ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa
nje zipatikane nchini.
Akizungumza hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya
ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo
kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua
katika uchumi wa viwanda.
“Serikali kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900
ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa
kati kwa kutumia viwanda”.alisema Mhe. Ummy.
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana
na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye
ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za
kemikali zitokananzo na dawa hizo.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane
na Taasisi ya viwango nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa
zisizokizi viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa
elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa
zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu .
Mbali na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa
ikusanye mapato kwa wingi zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga
hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA
Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe.
Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA
KAZI TU”.
“Tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri na nataka
kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye
kilele cha maendeleo na Afya bora” alisisitiza Dkt. Moses.
|
No comments:
Post a Comment