Na
Jonas Kamaleki
Serikali yajipanga kupunguza ajali za
barabarani kwa kiwango cha takribani asilimia 10 hapa nchini ili kupunguza vifo
na majeruhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuf Hamad Masauni kuwa baraza la Usalama Barbarani linakerwa
sana na kadhia ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
“Kukithiri kwa ajali za barabarani kwa siku
za hivi karibuni, umewezesha Baraza kuibuka na Mkakati wa Miezi Sita (6)
unaolenga katika kukabiliana na ajali za barabarani nchini, mkakati huu ni wa
muda mfupi kuanzia mwezi Agosti, 2016
hadi Februari 2017 tutakapokaa na kutathmini matokeo yake”, alisema
Masauni.
Masauni amesema ajali za barabarani
zimewaacha watoto wakiwa yatima na
kuwafanya akina mama kuwa wajane, hivyo
juhudi za makusudi inabidi zifanywe ili kupunguza kama sio kuondoa
kabisa ajali hizo.
Ametaja vyanzo vikuu vya ajali za
barabarani nchini kuwa ni pamoja na Makosa ya Kibinadamu, mazingira ya barabara
na ubovu wa vyombo vya moto.
Naibu waziri huyo amesema takwimu za ajali
barabarani katika miaka mitatu tangu 2012 ajali ziliongezeka toka 23,578 hadi
23, 842 kwa mwaka 2013, vifo vilikuwa 3,969 kwa mwaka huo hadi kufikia 1,043 mwaka
2013.
Vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka 2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama barabarani pamoja na juhudi zilizofanya na Baraza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka 2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama barabarani pamoja na juhudi zilizofanya na Baraza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Kwa mujibu wa Masauni, Mkakati
uliozinduliwa unalenga kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa
na ambayo husababisha kuongezeka kwa ajali za barabarani.
Ameyataja mambo hayo kuwa udhibiti wa
madereva walevi na kuendesha kwa uzembe, mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa
magari, uendeshaji magari bila sifa au leseni za udereva na Bima.
Masauni
ametaja mambo mengine katika Mkakati huu kuwa ni kudhibiti usafirisha wa
abiria kwa kutumia magari yasiyo na sifa kama vile Noaha na Probox, ajali za
pikipiki za magurudumu mawili (bodabaoda) na matatu (bajaj) na kuhakikisha
abiria wanafunga mikanda ya usalama wanapotumia vyombo vya moto kwa ajili ya
usafiri.
Maeneo mengine yatakayoangaliwa kwa mujibu
wa Masauni ni kuyabaini na kuyadhibiti maeneo tete na hatarishi ya ajali za
barabarani (Black spots/kilometres),
kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria za Usalama barabarani,
kuanza utaratibu wa Mfumo wa Nukta (point system) kwenye leseni za udereva,
kutoa mafunzo msasa kwa askari wa usalama barabarani na kutoa elimu na mafunzo
kwa bodaboda.
Ili kupunguza ajali za barabarani,
Masauni amasema Mkakati utadhibiti vitendo vya rushwa ambapo watoaji na wapokea
rushwa wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria, kuwapa tuzo askari wanaofanya vizuri
kuzuia ajali na kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria nay a mizigo, katika
kuutekeleza mkakati.




No comments:
Post a Comment