Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) aliyemaliza muda wa uwakilishi wake nchini Dk. Natalia Kanem (wa
pili kutoka kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) mara baada ya kufika Ofisini kwake kumuaga leo jijini Dar es salaam.Wengine
alioambatana nao ni Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na
Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez
(kulia) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) kuhusu machapisho mbalimbali ya Umoja yanayoelezea Maendeleo ya Tanzania leo jijini
Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini
hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa
Shirika hilo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.)akiangalia
moja ya chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021
alilokabidhiwa na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) , Mwakilishi Mkazi wa UNFPA anayemaliza
muda wake hapa nchini Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto), Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa
nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi
Msaidizi wa UNFPA (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja wakionesha chapisho la lenye Mipango ya Umoja
wa Mataifa mwaka 2016 -2021 leo jijini Dar es salaam.
Na.
Mwandishi Wetu - Dar
es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
(Mb.) amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini
hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa shirika hilo hapa nchini.
Akizungumza na mwakilishi huyo Ofisini kwake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimamia
kikamilifu utekelezaji wa Sera, miongozo na sheria mbalimbali zinazohusu usawa
wa jinsia na haki za watoto hususan watoto wa Kike.
Amesema
Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na UNFPA pamoja na mashirika
mengine ya Umoja wa Mataifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
jamii ya Tanzania.
Ameleza kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya
watoto linalohusisha ndoa na mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto linamalizika
katika jamii ya watanzania
Aidha,amesema
kuwa wizara yake itaendelea na juhudi za kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa
kuweka miundombinu na mazingira bora ya kujifungulia huku
akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuelimisha na kuhamasisha umma wa
watanzania juu ya umuhimu wa kuzingatia uzazi wa mpango.
Kwa upande wake Dk. Natalia Kanem ambaye alikua ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini
Tanzania, Alvaro Rodriguez ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano
iliyompatia katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini na kuahidi kuendeleza
kudumisha mashirikiano hayo atakapokuwa Makao Makuu ya Shirika hilo.
No comments:
Post a Comment